img

Rafiki wa Zari Azuia Mali za Ginimbi

November 24, 2020

MALI za aliyekuwa bilionea maarufu katika ukanda wa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika, Genius Kadungure ‘Ginimbi’ (36), zimezua balaa zito. Mwanamke aitwaye Zodwa Mkandla (46) ambaye anaelezwa kuwa mke halali wa bilionea huyo amezuia mgawanyo wa mali hizo.

 

 

Bilionea huyo raia wa Zimbabwe, ambaye alipata umaarufu kupitia mitandao ya kijamii kutokana na mtindo wake wa kuonesha maisha yake ya kifahari, anaelezwa kuwa na utajiri wa zaidi ya Sh bilioni 200.

 

Zodwa almaarufu Zozo ambaye ni rafi ki wa karibu wa mzazi mwenza wa mwanamuziki maarufu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ameelezwa kuwa chanzo cha kuchelewesha mgawanyo wa mali za bilionea huyo aliyepoteza maisha Novemba 8, mwaka huu katika ajali mbaya ya gari iliyochukua pia uhai wa rafi ki zake watatu.

 

 

Gazeti la Zim Morning Post limeeleza kuwa, siku chache baada ya mazishi ya bilionea huyo yaliyofanyika Novemba 14, mwaka huu, Zodwa ameibuka na kuanza kusuka mipango ya kurithi mali hizo hali iliyowawafanya wanafamilia wa Ginimbi kupigwa butwaa.

AJITETEA KUWA NI MKE HALALI

Licha ya kwamba mwanamke huyo alikiri kuwa hakuwa akiishi pamoja na Ginimbi tangu mwaka 2018, alifafanua kuwa bado alikuwa mke halali wa mwanaume huyo.

 

Zodwa ambaye ni mama wa kiroho wa mtoto wa Zari, Tiffah Dangote, ameeleza kuwa chanzo cha kutengana na mumewe huyo ni ‘ukicheche’ wa Ginimbi ambaye alikuwa mpenda totozi kupita kiasi.

 

Hata hivyo, Zim Morning Post limeeleza kwa kina kuwa, Zodwa ambaye ndiye mwanamke aliyempika Ginimbi na kuwa mafanikio makubwa kibiashara, mali za bilionea huyo hasa mashamba na jumba la Zimbabwe lililopo huko Domboshava, vyote vilikuwa vinamilikiwa kwa pamoja na wawili hao. Mbali na urithi huo, Zodwa aliwaeleza waombolezaji waliohudhuria mazishi ya bilionea huyo kuwa alikuwa yeye ndiye mwanamke pekee anayetambulika mke halali.

Akimzungumzia uhusuano wao, Zodwa anasema Ginimbi alikuwa mwanaume asiyetulia na mwanamke mmoja. Anasema kwa mara ya kwanza walianza safari yao ya mapenzi walipokutana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mugabe – Zimbabwe. “Ginimbi alikuwa ni mtu anayeonesha mapenzi ya kweli na alikuwa anajua kumjali mwanamke jambo ambalo siwezi kulisahau.

 

“Lakini ni kweli kuwa, Ginimbi alikuwa kiwembe kwelikweli, alikuwa anaweza kukuaminisha kuwa uko peke yako duniani. Sikuwahi kukutana na mwanaume anayejua kupenda kama huyu, kwa sababu anajua kuonesha upendo wa dhati kwelikweli wakati upande wa pili anachepuka vizuri tu,” anasema mwanamke huyo.

 

Zodwa alimsindikiza mumewe huyo kwa ujumbe aliouweka kwenye ukurasa wake mtandao wake wa Instagram, kwa kuandika kuwa; “Nenda ukampumzike salama mpenzi wangu, hakuna anayeweza kuelewa mimi na wewe tumeshirikiana nini, hakuna anayeweza kujaza nafasi yako moyoni mwangu, pumzika kwa amani mpenzi.”

WALIFUNGA NDOA?

Hata hivyo, wawili hao wanadaiwa kufunga ndoa ya kimila mwaka 2014, lakini ilibainika kuwa wamefarakana mwaka 2018 baada ya rafi ki yake Ginimbi, Wicknell Chivayo kumfi kisha mahakamani bilionea huyo kwa madai ya utapeli.

 

Zodwa mwenyewe aliandika katika ukurasa wake kipindi hicho kuwa; “Ni mume wangu, tuliishi pamoja, lakini Wicknell Chivayo alinipigia simu na kuniambia dada samahani nimempeleka mumeo mahakamani. “Licha ya changamoto anazopitia, ukweli utabaki kuwa ni mume wangu, ingawa kila mtu anaishi kivyake hilo haliwezi kuondoa uhalisi huo,” anasema.

 

Aidha, uhalali wa ndoa yao pamoja na umiliki wa mali hizo pia ulidhibitishwa na mahakama moja huko jijini Harare mwaka 2018, baada ya Zodwa kumburuza kortini mlinzi wa jumba hilo lao lililopo Domboshava.

 

Zodwa alidai kuwa mlinzi huyo aliyefahamika kwa jina la Justice Jasi alishiriki kumuibia pesa kiasi cha Sh milioni 139.1. Nyaraka zilizowasilishwa mahakamani, zilibainishwa kuwa jumba hilo, linamilikiwa na Zodwa pamoja na mumewe hali ambayo sasa inazidisha utata katika mgawanyo wa mali za bilionea huyo.

 

WANASHERIA WASEMA ATACHELEWESHA URITHI

Ujio huo wa Zodwa umeelezwa na wanasheria wa Ginimbi kuwa sasa utachelewesha mgawo wa mali za bilionea huyo. Wanasheria hao Brighton Pabwe pamoja na Jonathan Samkange ambao wote walikuwa wanasheria wa Ginimbi, walifafanua zaidi kuwa itachukua muda mrefu kutoa hadharani wosia rasmi wa jamaa huyo aliyejizolea umaarufu mitandaoni.

 

“Kwa sababu huyu alikuwa tajiri mkubwa na yapo mambo mengi ya kuweka sawa, hatuwezi kutoka hadharani na kuonesha wosia wake ilihali bado mambo hayajakaa sawa, kwa hiyo wafuasi wake wasubiri, lakini hatuwezi kusema kuwa ni lini,” alisema Pabwe.

 

ZARI ATUA KUMPA ‘SUPPORT’

Katika kile kilichoonekana kwenda kumuunga mkono rafi ki au shosti wake, Zari ametupia video zinazoonesha wawili hao wakitembelea kaburi pamoja na eneo ambalo Ginimbi alipata ajali. Hata hivyo, Zodwa amemshukuru Zari kwa kuamua kwenda Zimbabwe kumpa pole katika kipindi hiki kigumu.

ZODWA MKANDLA NI NANI

Zodwa ‘Mai Ginimbi’ Mkandla ni raia wa Zimbabwe ambaye pia anasifi ka kwa kuwa na utajiri kutokana na kujishughulisha na ujasiriamali, ikiwemo umiliki wa kampuni maarufu ya usafi ri katika ukanda huo wa Kusini -Traverze Travel. Zodwa ambaye sasa ana umri wa miaka 46, amezaliwa katika Kijiji cha Bubi kilichopo Mji wa Matabeleland nchini Zimbabwe.

 

Ana watoto wawili, Precious na Melisa ambao alizaa na mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Mutunzi. Baada ya kuachana na mwanaume huyo ndipo alipoangukia katika penzi la kijana huyo machachari, Ginimbi. Mwanamama huyo mwenye stashahada ya masuala ya usafi ri wa anga, ndiye anayetajwa kutaka kumiliki mali zote za bilionea huyo.

STORI: HARARE, ZIMBABWE

The post Rafiki wa Zari Azuia Mali za Ginimbi appeared first on Global Publishers.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *