img

Mpyagila akaribia kukalia kiti cha uenyekiti wa halmashauri ya Nachingwea

November 24, 2020

Ahmad Mmow, Nachingwea. 

Madiwani wa teule 40 wanaopitia Chama Cha Mapinduzi ( CCM) wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi leo wamemchagua diwani wa kata ya Mbondo, Adnani Mpyagila kuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea. 

Madiwani wateule hao 29 wa kata, 10 wa viti maalumu na mheshiwa mbunge wa jimbo la Nachingwea kupitia mkutano uliofanyika leo mjini Nachingwea katika ofisi ya CCM wilaya ya Nachingwea walimpa kura 28 diwani huyo. 

Aidha mwenyekiti aliyemaliza muda wake ambae ni diwani wa kata ya Ugawaji, Ahmad Makoroganya alipata kura 12. 

Huku Monica Kasembe ambae alijitoa katika kinyang’anyiro hicho hakupata hata kura moja. 

Aidha msimamizi wa uchaguzi huo ambae pia ni katibu wa CCM wa wilaya ya Nachingwea, Hakim Jackson alimtangaza diwani wa viti maalumu, Veronica Makota kuwa mgombea wa nafasi ya makamo mwenyekiti wa halmashauri hiyo katika baraza la madiwani. 

Nibaada ya kupata kura 31 dhidi ya 9 alizopata diwani wa kata ya Chiola, Mohamed Chiwalo. Huku Exavery Tambula ambae alijitoa kugombea hakupa kura hata moja. 

 Akizungumza baada ya kutangazwa matokeo hayo, Mpyagila licha ya kuwashukuru madiwani wenzake wa CCM kwa kumwamini aliahidi kuvunja kambi ambazo zilisababisha makundi. 

Alisema kwakushirikiana na madiwani wenzake iwapo atachaguliwa kuwa mwenyekiti atahakikisha makundi yote yanavunjwa na kuwana kundi moja litakalo kuwapelekea maendeleo wananchi kupitia halmashauri yao. 

 ” Atakaye sitahili kuwa kwenye kamati fulani atawekwa kwenye kamati husika kwa maslahi ya halmashauri na wananchi. Nisingependa halmashauri igawanyike kwasababu ya makundi. Tuwe wamoja ili tuwahudumia wananchi,” alisema Mpyagila. 

Kwakuzingatia idadi ya wajumbe wa baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Nachingwea lenye madiwani 50, wakati madiwani 40 wanapitia CCM na 10 Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) ni dhahiri Mpyagila na Makota wananafasi kubwa ya kushinda nafasi hizo. 

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu uliofanyika tarehe 28.10.2020 CCM kilishinda viti 29 vya udiwani kati ya 36 zilizopo wilayani Nachingwea. Hivyo kupata viti 10 vya viti maalumu. 

Huku mbunge wa jimbo la Nachingwea, Chinguile Amandus Julius akipitia Chama Cha Mapinduzi. 

Wakati CCM iliibuka mshindi katika kata 29, CHADEMA kilishinda kata saba ambazo vimekifanya kipate viti vitatu maalumu na kufanya kiwe namadiwani 10 ndani ya bazara la madiwani lijalo. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *