img

Mgogoro wa Ethiopia: Kiongozi wa Tigray Debretsion Gebremichael aapa kuendelea kupigana vita

November 24, 2020

Dakika 8 zilizopita

Mpiga Picha wa mji wa Tigray wa Humera anasema kwamba ameona watu wengi wakijeruhiwa katika ufyatulianaji wa risasi

Maelezo ya picha,

Mpiga Picha wa mji wa Tigray wa Humera anasema kwamba ameona watu wengi wakijeruhiwa katika ufyatulianaji wa risasi

Kiongozi wa eneo la Tigray nchini Ethiopia ametupilia mbali makataa ya waziri mkuu ya kujisalimisha kufikia leo Jumatano na ameahidi kuendelea kupigana katika vita vinavyokumba eneo la kaskazini mwa nchi.

Debretsion Gebremichael alikatakaa madai ya serikali kwamba mji mkuu wa eneo hilo Mekelle umezingirwa na vikosi vya serikali.

Mamia wamesemekana kuuawa huku makumi ya maelefu ya watu wakitoroka eneo hilo kwa karibu wiki tatu za mapigano.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa kuna uwezekano wa kutokea kwa mgogoro wa kibinadamu.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed Jumapili alitangaza saa 72 kwa wapiganaji wa eneo hilo kujisalimisha na jeshi limeonya wakazi wa Mekelle wapato 500,000 kuwa wanajeshi watazunguka mji huo na kuushambulia.

Lakini Bwana Debretsion, kiongozi wa chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF), alisema waziri mkuu “haelewi sisi ni kina nani. Ni watu na misimamo yetu na tuko tayari kufariki dunia tukitetea haki ya kutawala eneo letu”, Shirika la habari la AFP limemnukuu kiongozi huyo.

Chama cha TPLF kimekuwa kikitawala katika siasa za eneo hilo na kuna wakati kilikuwa kundi kubwa la waasi lenye nguvu na kuongoza mapigano ya kuondoa madarakani serikali iliyotangulia ya Ethiopia mwaka 1991.

Ramani ya Ethiopia

Kiongozi huyo wa Tigray pia alisema, kulingana na shirika la habari la Reuters, juu ya madai ya serikali ya mji wa Mekelle yalikuwa yanaziba ukweli baada ya jeshi kushindwa katika pande tatu.

Imekuwa vigumu kuthibitisha kile kinachoendelea katika eneo hilo kwasababu mawasiliano yamekatizwa.

Kipi kingine kilichtokea?

Serikali ya Ethiopia imeshtumu vikosi vua TPLF kwa kuharibu miundo mbinu ikiwemo uwanja wa ndege katika eneo la kale la Aksum ambalo ni kivutio cha utalii, tovuti ya habari ya Fana yenye kuhusishwa na serikali imesema.

Barabara iliofungwa

Chama cha TPLF hakijasema lolote kuhusu shutuma hizo lakini Bwana Debretsion ameliambia shirika la habari la Reuters Jumapili kuwa vikosi vyake vimefanikiwa kusitisha ya shuguli ya vikosi vya serikali ya kuendelea kuingia katika mji wao.

Je kuna majaribio yoyote ya kutafuta suluhu kwa njia kidiplomasia?

Nchi za Falme ya Kiarabu ni washirika wenye ushawishi mkubwa kwa serikali ya Ethiopia na zimeonesha kuwa na wasiwasi juu ya mapigano hayo na imejitahiji kuwasiliana na wengine Afrika pamoja na dunia nzima kwa jumla kumaliza vita hivyo.

Ijumaa, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kama mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, alitangaza uteuzi wake wa waliokuwa marais watatu kuwa wapatanishi na kumaliza vita hivyo.

Hatahivyo, Ethiopia ilikataa ofa hiyo kwasababu inachukulia oparesheni inayoendeleza kama shughuli ya ndani ya nchi.

“Hatujadiliani na wahalifu… Tunachohakikisha ni kuona wanakabiliwa na mkono wa sheria, wala sio kuwa nao katika meza ya mazungumzo,” Mamo Mihretu, msaidizi mwandamizi wa Bwana Abiy, ameiambia BBC.

Chanzo cha mapigano hayo ni nini?

Mgogoro huo umetokana na wasiwasi uliokuwepo kwa kipindi kirefu kati ya chama cha TPLF chenye nguvu zaidi eneo hilo na serikali kuu ya Ethiopia.

Debretsion Gebremichael

Bwana Abiy aliahirisha uchaguzi wa taifa kwasababu ya virusi vya corona mnamo mwezi Juni na wasiwasi uliokuwepo ukaendelea kulipuka.

Chama cha TPLF kinachukulia serikali ya Ethiopia kama isio halali na kusema kuwa Bwana Abiy hana tena mamlaka.

Chama hicho kilifanya uchaguzi wake ambao serikali inasema sio halali.

Novemba 4, Waziri Mkuu wa Ethiopia alitangaza oparesheni dhidi ya chama cha TPLF, akishutumu majeshi yake kwa kuvamia makao makuu ya jeshi eneo la kaskazini katika mji wa Mekelle.

Hata hivyo chama cha TPLF kimekanusha madai hayo.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *