img

Kiongozi wa waasi DR Congo afungwa kwa kutekeleza uhalifu dhidi ya binadamu

November 24, 2020

 

Aliyekuwa kiongozi wa wanamgambo katika taifa la jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo ubakaji wa watu wengi.

Mahakama ya kijeshi ilimpata Ntabo Ntaberi na hatia ya muaji, ubakaji, utumwa wa kingono na kuwasajili watoto walio chini ya miaka 15 katika jeshi lake.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo iliochukua takriban miaka miwili ambapo waathiriwa 178 walitoa ushahidi wao.

Umoja wa Mataifa unasema kwamba umauzi huo umeonesha ‘uzoefu wa kutenda uhalifu bila kujali una kikomo chake’.

‘Uamuzi huo unawapatia matumaini waathiriwa wa mzozo huo wa DRC , mateso waliopitia yamesikilizwa na kutambuliwa’, alisema Leila Zerrougui , mkuu wa ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa uliopo nchini DR Congo.

Ntaberi anayejulikana kama Sheka , alikuwa mmoja wa viongozi wa kundi moja la wapiganaji kwa jina Nduma of Congo{NDC} ambalo lilifanya operesheni zake katika mkoa wa mashariki wa Kivu.

Eneo la mashariki mwa DRC limezongwa na mizozo , iliochochewa na migawanyiko ya kisiasa mbali na utajiri wa raslimali katika eneo hilo.

Kulikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini DR Congo kati ya 1998 na 2003, lakini baadhi ya wapiganaji wanendelea kupigana mbali na kusababisha mateso katika eneo hilo ambapo uujumbe wa UN unatatizika kuleta amani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *