img

JPM afanya uteuzi mwingine

November 24, 2020

Rais Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamesd Shein, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta, ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa hii leo Novemba 24, 2020, kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, ambapo pia Rais Magufuli, amemteua Dkt. Harrison Mwakyembe, aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), akichukua nafasi ya Mariam Joy Mwaffisi.

Mwingine aliyeteuliwa hii leo ni aliyewahi kuwa Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), akichukua wadhifa huo kwa kipindi cha pili sasa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *