img

Japan, China zakubaliana kurejesha safari za kibiashara

November 24, 2020

 

Japan na China zimekubaliana leo kuanzisha tena safari za kibiashara kati ya nchi hizo mbili ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wakati kukiwa na janga la virusi vya corona. Hayo ni kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Japan Toshimitsu Motegi. 

Motegi na mwenzake wa China Wang Yi, aliyewasili Tokyo mapema leo kwa ziara ya siku mbili, wameamua kuondoa vikwazo vya usafiri vilivyowekwa kupambana na janga la corona licha ya ongezeko la karibuni la maambukizi nchini Japan. 

Sekta za kiuchumi na utalii nchini Japan zimeathirika pakubwa na janga hilo hasa tangu safari za ndege zilipositishwa kutokana na mripuko wa virusi hivyo mapema mwaka huu. 

Wakati wa mazungumzo ya leo, Motegi amemuomba Wang kuzizuia meli za Kichina za walinzi wa pwani kuingia katika visiwa vinavyodhibitiwa na Japan katika Bahari ya Mashariki mwa China, ambavyo vimekuwa chanzo cha mivutano ya kidiplomasia.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *