img

Hadi Raha! Mapacha Waoana Siku Moja

November 24, 2020

Hassan Sulaiman na Hussaini Dey ni mapacha wawili wa kiume wenye miaka 33, wameoa mapacha wenzao wa kike ambao wamefahamika kwa majina ya Hassana na Hussaina huko Kano Kaskazini mwa nchi ya Nigeria.

 

Mmoja wa mapacha wa kiume Hassan Sulaiman amesema tangu walivyokuwa wadogo walikuwa wanasema kitu bora kwao ni kuoa mapacha wenzao ambapo wametimiza ndoto zao.

“Tangu tulipokuwa wadogo, tulikuwa tunafanya kila kitu pamoja, tulikuwa tunavaa nguo zinazofanana, kula chakula cha aina moja na tulisoma katika darasa moja, hata tulipoenda kusomea masuala ya afya namba ya usajili wa mtihani yake ilikuwa 010 wakati yangu ilikuwa 011.”

Aidha ameongeza kusema, “Kwa muda mrefu tulipanga kuoa mapacha na hata familia yetu walituambia tuoe mapacha, kabla ya sasa, tumekuwa tukijaribu bahati yetu na sasa tuna furaha sana ndoto zetu zimetimia”.

The post Hadi Raha! Mapacha Waoana Siku Moja appeared first on Global Publishers.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *