img

Biden ataja timu yake ya usalama wa taifa na kidiplomasia

November 24, 2020

Rais mteule wa Marekani Joe Biden ametaja timu yake ya juu ya kidiplomasia na usalama wa kitaifa kwa utawala wake ujao Jumatatu, ikiwa ni pamoja na mmoja wa washauri wake wa karibu zaidi wa maswala ya kigeni, Antony Blinken, kuwa waziri wa mambo ya nje ya nchi.

Biden pia alimtaja mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati mmoja John Kerry, kwa nafasi mpya kama mjumbe maalum wa rais wa hali ya hewa wakati akiwa anashikilia kiti kwenye Baraza la Usalama la Kitaifa. Hii inaonyesha ni jinsi gani utawala ujao wa Biden ulivyojipanga kushughulikia , mabadiliko ya mabadiliko ya hali ya hewa kama suala la haraka la usalama wa kitaifa ilieleza ofisi yake ya mpito.

Biden akiwa anajiandaa kuwa rais wa 46 wa Marekani na akiwa na umri wa miaka 78, atakuwa rais mwenye umri mkubwa zaidi, wakati wa kuapishwa kwake Januari 20, huku Rais Donald Trump akiwa anaendelea na jaribio lake la kisheria la muda mrefu la kutengua ushindi wa uchaguzi wa Novemba 3 wa kidemokrasia.

Biden, akisimamia mabadiliko yake ya kuingia madarakani Washington kutoka nyumbani kwake Wilmington, Delaware, alimchagua Alejandro Mayorkas kama waziri wa usalama wa ndani ya Nchi. Mwanasheria Mmarekani mwenye asilia ya Cuba, yeye ni naibu waziri wa zamani wa wizara hiyo , na ikiwa atathibitishwa na Seneti, atakuwa kiongozi wake wa kwanza wa Kilatino na mhamiaji.

Biden pia amemtaja mwanadiplomasia mkongwe Linda Thomas-Greenfield kujiunga na Baraza lake la Mawaziri linalokuja kama chaguo lake kwa nafasi ya Balozi kwenye Umoja wa Mataifa .Nafasi hiyo inahitaji uthibitisho wa baraza la Seneti.

Linda Thomas-Greenfield amefanya kazi katika tawala zote za wademokrat na Warepublican wakati wa miaka 35 ya kazi katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani.Akiwa mtaalam wa masuala ya Afrika, aliwahi kuwa Balozi wa Marekani nchini Liberia, na alishikilia wadhifa hupo pia katika nchi za Kenya, Gambia na Nigeria. Chini ya Rais Barack Obama, aliwahi kuwa naibu waziri anayeshughulika na maswala ya Afrika (2013-2017), akiendeleza na kusimamia sera ya Washington kuelekea bara la Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara. Amefanya kazi pia huko Geneva katika Ujumbe wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa.

Imetayarishwa na Sunday Shomari,VOA Washington Dc

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *