img

Waziri mkuu wa Israel afanya mazungumzo ya siri Saudi Arabia

November 23, 2020

Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu at a news conference in Jerusalem on 19 November 2020

Maelezo ya picha,

Ofisi ya waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu hajathibitisha taarifa hizo

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameenda Saudi Arabia kwa siri siku ya Jumapiliili kukutana na mwana mfalme Mohammed Salman, vyombo vya habari vya Israeli vimeripoti.

Taarifa za ndege zinaonesha kuwa bwana Netanyau alitumia ndege ya biashara kusafiri kupitia eneo la bahari ya Red Sea katika mji wa Neom.

Hakuna taarifa rasmi zilizothibitisha , lakini waziri wa Israeli aliambiwa kuhusu suala hilo na waziri wa masuala ya nje.

Huu utakuwa mkutano wa kwanza wa viongozi ambao wana kihistoria ya uadui ambao Marekani inataka wapatane.

Hivi karibuni rais Donald Trump amesitisha mkataba wa kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Israel na United Arab Emirates, Bahrain na Sudan.

Saudi Arabia ilipokea wito huo huku ikiwa na wasiwasi lakini ilisema haitafikia maridhiano mpaka amani ipatikane kati ya Waisrael na Wapalestina.

Akinukuu vyanzo vya habari ambavyo havikutaka ktajwa majina yao , Chombo cha habari cha umma cha Israeli Kan na vyombo vingine vya habari vimeripoti kuwa waziri mkuu Netanyahu na kiongozi wa huduma ya inteligensia ya Mossad, Yossi Cohen, alifanya mazungumzo siku ya Jumapili na mwana mfalme Mohammed na waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo.

Mkutano ulifanyika mjini Neom, katika eneo la kivutio cha watalii cha Saudi Arabia, kaskazini mwa pwani ya Red Sea 70km (40 miles) kutoka kusini mwa Israel, vyanzo hivyo vimeeleza.

Kwa mujibu wa data kutoka rada -FlightRadar24.com, zinasema kuwa ndege hiyo ya binafsi ya Gulfstream IV iliondoka Tel Aviv katika uwanja wa kimataifa wa Ben Gurion majira ya 17:40 GMT Jumapili na kuelekea kusini mashariki mwa pwani ya Misri kabla ya kuelekea Saudi Arabia katika pwani ya Red Sea.

1px transparent line

Ndege hiyo ilitua Neom baada ya saa 18:30 GMT na kubaki chini mpaka 21:50, kwa mujibu wa data. Na kurejea Tel Aviv kwa kutumia njia ileile.

Vyombo vya habari vya Israeli vimeripoti kuwa ndege hiyo inamilikiwa na mfanyabiashara Udi Angel na bwana Netanyahu alitumia ndege hiyo katika misafara mingine iliyopita.

Hakuna taarifa rasmi zilizothibitisha kuhusu mkutano wa waziri mkuu, waziri wa Israeli Zeev Elkin taliiambia Radio ya jeshi: “Sikuwa katika ndege hiyo kwenda Saudi Arabia.”

Mshauri wa masuala ya mitandao ya kijamii wa Netanyahu, Topaz Luk, alisema kuwa hakuna suala kama hilo, aliandika katika tweeter: “Gants anafanya siasa lakini waziri mkuu anataka amani”.

US Secretary of State Mike Pompeo (L) speaks to Saudi Crown Prince Mohammed bin Salman (R) (22 November 2020)

Maelezo ya picha,

Mike Pompeo (kushoto) na Mwana mfalme wa Saudi Mohammed bin Salman (kulia)

Bwana Luk alionekana akinukuu maamuzi ya waziri wa ulinzi Benny Gantz, kuwa mpinzani wa bwana Netanyahu’alitoa madai ya tuhuma kubwa za rushwa katika historia ya Israel.

Chombo cha habari cha taifa cha Saudi kimeripoti kuwa mwana mfalme Mohammed alipanga kukutana na bwana Pompeo mjini Neom, siku ya Jumapili usiku lakini hakutaarifu kuhusu ujio wa bwana Netanyahu.

Rais Trump alisema wataalamu wa Saudi Arabia inabidi waweke jitihada za kuboresha mahusiano na Israel.

Waziri wa mambo ya nje mwana mfalme Faisal bin Farhan Al Saud alisema kwenye mahojiano na wakala wa habari wa Reuters wakati wa mkutano wa G20 , siku ya Jumamosi kuwa nafasi ya ufalme haijabadilika.

“Tumekuwa tukiunga mkono kwa muda mrefu jitihada za kuleta uhusiano wa amani kati ya Israel na mataifa ya kiarabu.”

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *