img

VIDEO: Kampuni ya JATU yaorodheshwa kwenye soko la hisa Dar

November 23, 2020

Mtendaji mkuu wa Masoko, Nicodemus Mkama, ameipongeza kampuni ya JATU PLC kwa kuzalisha ajira zaidi ya Elfu Kumi huku wengi wao wakiwa wanawake na wakina mama…

Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) CPA Nicodemus Mkama,  leo jjini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa hisa za JATU Plc katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE.)

“Nawashukuru wadau wa sekta ya fedha kwa kuhudhuria hafla hii ya kuorodheshwa kwa hisa za Kampuni ya JATU PLC kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, huu ni uthibitisho kwamba sekta ya fedha ina wadau wengi wanaounga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli iliyoweka mazingira wezeshi ya kiutendaji yenye malengo ya kukuza uwekezaji kupitia masoko ya mitaji.” Ameeleza Mkama.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI…..USISAHAU KUSUBSCRIBE

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *