img

Ulaya yatishia kuchukua hatua dhidi ya watakao hujumu amani ya Libya

November 23, 2020

 

Nchi za Ulaya zinazojihusisha na juhudi za kumaliza mgogoro wa Libya, zimeonya kuwekea vikwazo pande zozote zitatakazohujumu mchakato huo hafifu wa amani, zikisema ziko tayari kuchukua hatua yoyote dhidi ya yeyote atakayezuia mazungumzo.

Kwenye taarifa ya pamoja, Ujerumani, Uingereza na Italia zimehimiza pande zinazohasimiana Libya pamoja na washirika wao kimataifa kujiepusha na juhudi zozote tofauti zisizo na utaratibu tofauti, zinazoweza kuhujumu juhudi zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa. 

Taarifa hiyo haikutaja washirika wengine kwenye onyo lao, lakini hapo nyuma, zimezishutumu Urusi na Uturuki kuingilia kati masuala ya ndani ya Libya.

Nchi hizo nne za Ulaya zimesema zimeukaribisha uamuzi wa pande hasimu Libya kuandaa uchaguzi mkuu Disemba 24 mwaka 2021.

Urusi imeshutumiwa kwa kuwaunga mkono mamluki wanaopambana na serikali ya kitaifa (GNA) iliyoko Tripoli inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, nayo Uturuki imewatuma wanajeshi wake kuiunga mkono GNA.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *