img

Ujerumani, Uingereza na Ufaransa kujadili mkataba wa nyuklia wa Iran leo

November 23, 2020

 

Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Heiko Maas, anafanya mkutano leo na wenzake wa Uingereza na Ufaransa mjini Berlin kuhusu mazungumzo yanayoangazia mkataba wa nyuklia na Iran.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Ujerumani amesema hayo na kuongeza kuwa Iran inakiuka makubaliano kwa utaratibu.

Msemaji huyo ameongeza kuwa pamoja na washirika wao, wameitaka Iran kuacha kuukiuka mkataba huo na ianze kuyatimiza masharti na ahadi zake kwa mujibu wa makubaliano hayo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *