img

‘Ndoto yetu ni kuolewa na mapacha kama sisi’

November 23, 2020

Di twins for dia pre-wedding shoot

Mapacha wanaofanana wenye miaka 33, Hassan Sulaiman Indabawa na Hussaini dey wameoa siku moja mapacha wanaofanana Hassana Ado Ashir na Hussaina huko Kano magharibi mwa Nigeria siku ya Ijumaa, Novemba 20.

Ni tukio la nadra kwa mapacha waliozaliwa siku moja kuolewa au kuoa na mapacha wengine waliozaliwa siku kama yao.

Hassan ameiambia BBC kuwa tangu walipokuwa wadogo wanakuwa yeye na ndugu yake walikuwa wanazungumzia kuwa jambo zuri kwao ni kuoa mapacha .

“Tangu tulipokuwa wadogo, tulikuwa tunafanya kila kitu pamoja, tulikuwa tunavaa nguo zinazofanana, kula chakula cha aina moja na tulikuwa darasa moja darasani mpaka tulipoenda kusomea masuala ya afya na namba ya mtihani yake ilikuwa 010 wakati yangu ilikuwa 011.”

“Kwa muda mrefu tulipanga kuoa mapacha na hata familia yetu walituambia tuoe mapacha, kabla ya sasa.

Tumekuwa tukijaribu bahati yetu na sasa tuna furaha sana ndoto zetu zimetimia ” Hassan alisema.

Di twins for dia pre-wedding shoot

Hassan alikutana na mpenzi wake katika harusi ya kaka yake mkubwa ndio wakakutanishwa na wadada hao.

“Kwa miezi mitatu ya kukutana nao, tulikuwa hatujawaona kabisa mpaka tulipokutana sasa na tunawaona wako kama sisi, tunamshukuru Mungu sana , na wao pia wamekuwa wakifanya kila kitu pamoja.”

Mimi nitakuwa bibi harusi , Hassana aliiambia BBC na ana furaha sana kuwa dada yake pia anaolewa na pacha mwingine.

Di twin grooms

“Hakuna maneno yanayoweza kueleza furaha yangu, kueleza jinsi ninavyojisikia. Nilikuwa naomba sana kuolewa na mapacha tangu nikiwa mdogo na nina furaha ndoto yangu imetimia, ninamshukuru Mungu kwa hilo.”

Pacha mwingine Hussaini alisema umoja ni jambo muhimu sana,alikuwa anafurahi kuona mapacha wanamuziki walivyokuwa na umoja.

“Umoja kwa mapacha ni jambo muhimu sana, tumeona kile kilichotokea kwa wanamuziki P square walikuwa mapacha kama sisi na walikuwa na furaha wakati wanafanya kila kitu kwa pamoja.”

Hassana and Hussaina

Hatimaye nimekuwa bibi harusi, Hussaina mwenye umri wa miaka 23 , anasema ni jambo muhimu sana kwake na dada yake.

“Tumekuwa pamoja, tumesoma pamoja tangu shule ya msingi mpaka chuo, tumelala kitanda kimoja na sasa tunaenda kubadili maisha yetu kwa kuwa na pacha wengine…” alizungumza akiwa anatabasamu.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *