img

Mtu mmoja afariki baada ya kushambuliwa na papa baharini Australia

November 23, 2020

Mtu mmoja ameripotiwa kupoteza maisha baada ya kushambuliwa na papa katika pwani ya Cable Beach iliyoko magharibi mwa Australia.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 55 aliyetolewa baharini akiwa amejeruhiwa vibaya na papa, alifariki papo hapo.

Baada ya tukio hilo, eneo la pwani lilifungwa kwa muda na wananchi kuzuiwa kuingia baharini kama mojawapo ya hatua ya tahadhari za kiusalama.

Katika nchi ya Australia, kumekuwa na mashambulizi 22 ya papa ndani ya mwaka huu pekee yaliyosababisha vifo vya watu 8.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *