img

Maelfu wakosa kupiga kura nchini Burkina Faso kutokana na hofu za kiusalama

November 23, 2020

Mamia kwa maelfu ya wapiga kura nchini Burkina Faso hawakuweza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa jana kutokana na vitisho vya usalama, wakati taifa hilo la Afrika Magharibi likipambana na uasi unaoongezeka wa itikadi kali. Idadi isiyofahamika ya wanajeshi waliwekwa katika maeneo mbalimbali kutoa ulinzi katika uchaguzi wa rais na bunge, ambao unatarajiwa kumpa ushindi Rais Roch Marc Christian Kabore wa kuongoza kwa muhula wa pili wa miaka mitano.

Lakini hakuna kura zilizopigwa katika maeneo makubwa ambayo yako nje ya udhibiti wa serikali na ambayo hushambuiwa karibu kila siku na wanamgambo wa itikadi kali. Tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa idadi Fulani ya vituo vya kupiga kura za urais vilifungwa baada ya kupokea vitisho.

Kati ya watu 300,000 na 350,000 hawakupiga kura

Burkina Faso Wahlen 2020 | Sicherheitskräfte

Wapiga kura wakishiriki zoezi kwa ulinzi mkali

Rais wa tume hiyo Newton Ahmed Barry baadae akawaambia wanahabari kuwa kati ya watu 300,000 na 350,000 ya karibu wapiga kura milioni 6.5 hawakupiga kura zao kutokana na vitisho vya usalama.
Baada ya kupiga kura yake jana mjini Ougadougou, Rais Kabore alipinga tuhuma za upinzani za kuwepo wizi wa kura.  Lakini mtalaamu wa siasa Drissa Traore anasema Kabore bado ana nafasi kubwa dhidi ya upinzani ambao haujafanikiwa kuungana nyuma ya mgombea mmoja.

Washindani wawili wakuu wa Kabore ni mgombea aliyemaliza wa pili katika uchaguzi wa 2015, kiongozi mkongwe wa upinzani Zephirin Diabre na Eddie Komboigo, anayegombea kwa chama cha rais wa zamani Blaise Compaore. Compaore aliyeondolewa madarakani kupitia vuguvugu la umma mwaka wa 2014 baada ya miaka 27 madarakani, sasa anaishi uhamishoni.

Malalamiko ya wizi wa kura katika mchakato wa uchaguzi

Diabre amewaambia wanahabari kuwa “kulikuwa na operesheni kubwa iliyoongozwa na walio madarakani ya kufanya wizi mkubwa wa kura” ili kumpa Kabore ushindi katika duru ya kwanza. Mkuu wa chama cha rais, Simon Compaore amepinga madai ya Diabre akisema Kabore hahitaji uchakachuaji wa aina yoyote ili kushinda uchaguzi.

Soma zaidi: HRW: Makaburi ya halaiki yagunduliwa Burkina Faso

Kabore anaweza kuepuka duru ya pili kwa kushinda zaidi ya asilimia 50 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa jana – kama alivyofanya katika mwaka wa 2015. Machafuko yanayohusiana na wanamgambo wa itikadi kali yamewalazimu watu milioni moja – ikiwa ni asilimia tano ya jumla ya idadi ya watu milioni 20 – kukimbia makwao katika miaka miwili iliyopita na karibu 1,200 kuuawa tangu 2015.

Chanzo: AFP

 

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *