img

Kilo 3,195,337 za korosho zanunuliwa RUNALI

November 23, 2020

Na Ahmad Mmow, Ruangwa. 

Jumla ya kilo 3,195,337 zimeuzwa na chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, kilichopo mkoani Lindi kupitia mnada wa saba kwa msimu 2020/2021 uliofanyika leo mjini Ruangwa. 

Katika mnada huo wa saba kwa RUNALI na wakumi na nne kwa mkoa wa Lindi wenye vyama vikuu viwili ( RUNALI na Lindi Mwambao ) ulikuwa na barua 14 za wanunuzi walioomba kununua korosho ghafi hizo. 

Katika ghala la Lipande ambalo lina tani 409 na kilo 601 bei ya juu na chini ilikuwa shilingi 2,530 ambazo zimenunuliwa na kampuni ya Udhaya. 

Aidha katika ghala la Export lenye tani 390 na kilo 944  bei ya juu ni shilingi 2,530 kwa kila kilo moja. Ambapo kampuni ya Udhaya imenunua korosho zote. Huku katika ghala la Lindi farmers lenye tani 563 na kilo 968 kampuni hiyo ya Udhaya imenunua korosho zote kwa bei ya shilingi 2,530 kwa kila kilo moja. 

Katika ghala la Pachani lenye tani 619 na kilo 968, kampuni za Udhaya na MGM Commodities zimefanikiwa kununua korosho hizo kwa bei ya juu ya shilingi 2,537 na bei ya chini shilingi 2,515 kila kilo moja. 

Mbali na maghala hayo, katika ghala la Umoja lenye tani 1,211 na kilo 250 kampuni za RBST na Sibatanza zimefanikiwa kununua korosho hizo kwa bei ya juu ya shilingi 2,412 na bei ya chini ni shilingi 2,352 kwa kila kilo moja. 

Akizungumza baada ya wakulima kuridhia kuuza kwa bei hizo, mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa alitoa wito kwa wakulima na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika ( AMCOS ) washirikiane bega kwa bega kuzuia korosho chafu ziingizwe kwenye maghala na kuharibu ubora wa zao hilo. 

Alisema wakulima hawatakiwi kubweteka baada ya kuona bei zinaongezeka bali waendelee kulinda ubora. ¥ Wito wa Mgandilwa ambae pia aliwaomba wakulima kuchangamkia bei hizo kwakupeleka korosho maghalani yaliungwa mkono na mwenyekiti wa RUNALI, Hassan Mpako.

Mpako alisema wakulima hawanabudi kulinda ubora wa zao hilo. Kwani bei nzuri haziji kwa miujiza, bali zinatokana na ubora. 

Alisema katika kipindi hiki ambacho mvua zinatarajiwa kuanza kunyesha, ni vizuri waanike walau kwa siku nne kabla ya kupeleka maghalani. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *