img

Ethiopia yasema uwanja wa ndege wa Axum umeshambuliwa

November 23, 2020

 

Vikosi vya jimbo la kaskazini mwa Ethiopia Tigray, vijulikanavyo kama Ukombozi wa Watigray-TPLF, vimeharibu uwanja wa ndege katika mji wa zamani wa Axum. 

Shirika la habari linaloshirikiana na serikali limeripoti hayo leo baada ya vikosi vya serikali ya shirikisho vinavyoendelea kuukaribia mji mkuu wa Tigray Mekelle kuwapa muda wa saa 72 kusalimu amri. 

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, amevitaka vikosi vya TPLF kusalimu amri ifikapo Jumatano la sivyo wafanye mashambulizi katika mji huo. 

Hata hivyo kiongozi wa TPLF Debretsion Gebremichael ameliambia shrike la habari la Reuters kwamba serikali ya shirikisho inatumia vitisho kama kinga na kuwawezesha kukusanyika baada ya kushindwa katika ngome tatu.

Hakukuwa na kauli kutoka pande zote mbili kuhusu madai ya hivi karibuni na hivyo shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha kauli hizo.

Miito ya Umoja wa Mataifa, kutoka Afrika na Ulaya kutaka mazungumzo yafanywe kusuluhisho mgogoro huo haijazaa matunda.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *