img

Chanjo ya AstraZeneca ina ufanisi wa asilimia 90

November 23, 2020

AstraZeneca leo Jumatatu imesema majaribio ya hatua za mwisho ya chanjo yake dhidi ya virusi vya corona imeonyesha ufanisi hadi wa hadi  90%, kampuni hiyo imesema  maafisa wa Afya wa umma wawe na matumai kuwa hivi karibuni wanaweza kupata chanjo ambayo ni bei nafuu na rahisi kusambaza kuliko kampuni nyengine za dawa.

Matokeo ya chanjo hio yanatokana na uchambuzi wa muda wa majaribio nchini Uingereza na Brazil, chanjo hiyo imetengenezwa kwa ushirkiano wa Chuo Kikuu cha Oxford na kampuni ya dawa AstraZeneca. Inaarifiwa kuwa miongoni mwa waliopokea chanjo hiyo wakati wa majaribio hakuna aliyelazwa hospitalini au kuwepo kwa visa vikali vya COVID-19. Soma zaidi Merkel ana wasiwasi na utolewaji sawa wa chanjo ya COVID-19

Kampuni ya AstraZeneca imesema kufikia mwisho mwa 2020 itakua imetengeneza dozi milioni 200, ambayo ni mara nne zaidi ya mshindani wake mkuu Pfizer. 

Coronavirus Impfstoff Symbolbid

Sindano inayoonyesha chanjo ya Corona

Usalama na ufanisi

Ufanisi na usalama wa chanjo hii inathibitisha kuwa itakuwa bora sana dhidi ya COVID-19 na itakuwa na athari ya haraka kwa dharura hii ya afya ya umma,” amesema mtendaji mkuu wa AstraZeneca Pascal Soriot.

Kampuni ya AstraZeneca imesema chanjo yao inaweza pia kusafirishwa na kuhifadhiwa kwenye friji ya kawaida, ambayo watetezi wake wanasema ingeifanya iwe rahisi kusambaza, haswa katika nchi masikini, kuliko Pfizer, ambayo inahitaji kusafirishwa na kuhifadhiwa kwa kiwango cha joto nyuzi 70 kipomo cha Celsius.

Taarifa zinasema kuwa Chuo Kikuu cha Oxford na AstraZeneca zitatoa chanjo hiyo kwa $2.50 kila dozi wakati ambapo Pfizer ilisema itatoa dawa hio kwa $20 kwa kila dozi na Kampuni ya Moderna itatoza $15 hadi $25 kulingana na kampuni zitakazokubali kusambaza chanjo hiyo. Nchi za G20 kuhakikisha haki katika ugavi wa chanjo ya corona

kampuni hiyo ya dawa sasa inasema inaendelea na mikakati ya kuomba kuruhiswa kuanzisha kutumika kwa chanjo hio na itahitaji ruhusa ya dharura kutoka kwa sshirika la Afya Duniani WHO, ili kupata ruhusa ya kusambaza chanjo hio katika matiafa yenye kipato cha chini.

Brasilien I Coronavirus Impfung

Daktari akimdunga mtu sindano ya Chanjo ya Corona kwa ajili ya majaribio

“Habari juu ya matokeo ya chanjo ya COVID-19 ya AstraZeneca ni ya kutia moyo na tunatarajia kuona data kama tunavyofanya na matokeo mengine”, amesema mwanasayansi mkuu wa Shirika la Afya Duniani Soumya Swaminathan.

huku hayo yakijiri  kuna wasiwasi kwamba nchi kama Uingereza, Marekani , Ujerumani na Ufaransa tayari zimefanya mazungumzo ya moja kwa moja na makampuni ya dawa, ikimaanisha kwamba kiwango kikubwa cha chanjo tayari kimechukuliwa.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema ana wasiwasi kwamba hakuna makubaliano makubwa ya chanjo ambayo yamefikiwa na mataifa maskini hata wakati nchi tajiri zikinunua dozi kubwa kutoka makampuni ya dawa.

 

Rtre/AP

 

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *