img

KMC wataja siri ya chapa chapa yao, on September 23, 2020 at 8:01 am

September 23, 2020

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM UONGOZI wa KMC, umetaja  siri ya kikosi chao kufanya vizuri katika michezo yake mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kuwa ni wachezaji kujituma na kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja. KMC inaiongoza msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi tisa, baada ya kupata ushindi kwenye michezo yake yote,

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa KMC, umetaja  siri ya kikosi chao kufanya vizuri katika michezo yake mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kuwa ni wachezaji kujituma na kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja.

KMC inaiongoza msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi tisa, baada ya kupata ushindi kwenye michezo yake yote mitatu iliyoshuka dimbani.

Timu hiyo inayomilikiwa na Manispaa ya Kindononi katika Jiji la Dar es Sa laam, ilizindua msimu kwa kishindi baada ya kuilaza Mbeya City mabao 4-0, ikailaza Tanzania Prisons mabao 2-1(michezo yote ikichezwa Uwanja wa Uhuri, Dar es Salaam) kabla ya kuitungua Mwadui mabao 2-1, Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Akizungumza na MTANZANIA, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema kuwa kila mchezaji wao anatambua majukumu yake na kutimiza kwa wakati jambo linalowapa matokeo chanya.

“Wachezaji wanatambua kwamba nini kinahitajika ndani ya timu na wao hesabu zao ni kuona wanapata ushindi hiyo ndiyo furaha yao pia.

“Kwa kufanya hivyo kunawafanya wawe na nguvu katika kupambana na kupata matokeo na hicho ndicho ambacho kinatokea, tupo na tunazidi kupambana zaidi na zaidi,”alisema.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *