img

KOLABO YA ALICIA KEYS, DIAMOND YAUGUSA UBALOZI WA MAREKANI, on September 21, 2020 at 9:53 am

September 21, 2020

 CHRISTOPHER MSEKENA  WIMBO Wasted Energy ambao staa wa Marekani, Alicia Keys, amemshirikisha Diamond Platnumz, umeendelea kufanya vizuri kiasi cha kuugusa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.  Mapema jana Ubalozi wa Marekani ulitumia ukurasa wake wa Twitter kutoa ujumbe wa kufurahishwa na kolabo hiyo kwa kusema: “Inafurahisha kuona msanii wa Marekani Alicia Keys akimshirikisha msanii wa Kitanzania,

 CHRISTOPHER MSEKENA 

WIMBO Wasted Energy ambao staa wa Marekani, Alicia Keys, amemshirikisha Diamond Platnumz, umeendelea kufanya vizuri kiasi cha kuugusa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania. 

Mapema jana Ubalozi wa Marekani ulitumia ukurasa wake wa Twitter kutoa ujumbe wa kufurahishwa na kolabo hiyo kwa kusema: “Inafurahisha kuona msanii wa Marekani Alicia Keys akimshirikisha msanii wa Kitanzania Diamond Platnumz, goma jipya la Wasted Energy ni moto.” 

Aidha, Alicia Keys ameshangazwa na mapokezi makubwa ya wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube ambapo umesikilizwa mara nyingi zaidi kuliko ngoma yoyote kwenye albamu yake, ALICIA. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *