img

Tuzingatie ilani za vyama ili tufanye maamuzi Oktoba 28,on September 17, 2020 at 7:48 am

September 17, 2020

DK. HELEN KIJO-BISIMBA TUKO katika kipindi muhimu sana ya ratiba ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Tumepita katika hatua nyingi kuelekea uchaguzi huu. Katika hivyo vipindi vilivyopita tuliona mambo mengi, lakini sasa tuko katika  kipindi cha karibu na mwisho kufikia uchaguzi wenyewe. Kwa wale waliojiandikisha na hata ambao hawajajiandikisha, inapaswa kufuatilia kampeni zinazoendelea. Umuhimu wa
The post Tuzingatie ilani za vyama ili tufanye maamuzi Oktoba 28 appeared first on Gazeti la Rai.,

DK. HELEN KIJO-BISIMBA

TUKO katika kipindi muhimu sana ya ratiba ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Tumepita katika hatua nyingi kuelekea uchaguzi huu. Katika hivyo vipindi vilivyopita tuliona mambo mengi, lakini sasa tuko katika  kipindi cha karibu na mwisho kufikia uchaguzi wenyewe.

Kwa wale waliojiandikisha na hata ambao hawajajiandikisha, inapaswa kufuatilia kampeni zinazoendelea. Umuhimu wa kampeni ni kwamba kila mgombea kuanzia wa udiwani, ubunge hadi urais kuelezea maono ya chama chake iwapo kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi kwa miaka mitano ijayo.

Tunafahamu hakuna mgombea asiyetokana na chama kimojawapo cha siasa kwa vile kwa mujibu wa Katiba tuliyonayo kila mgombea anapaswa kutokana au kudhaminiwa na chama cha siasa.

Kila chama kimeandaa ilani yake ambayo ndio inaongoza kutoa mwelekeo wa yale chama hicho kitakachotekeleza na kusimamia kikiwa madarakani. Wagombea wanapaswa kuwaeleza wapiga kura watarajiwa kilichopo kwenye ilani ili kuwashawishi kuwapigia kura.

Na wapiga kura wanapaswa kuzielewa ilani hizo ili kufanya maamuzi pamoja  na kuwafahamu hao walioteuliwa na vyama vyao iwapo wana uwezo wa kusimamia au kutekeleza yaliyomo katika ilani hizo.

Ilani huwa ndio kipimo au kama nilivyomsikia mmoja wa wagombea akisema ni agano wanalotaka kulifunga na wananchi kuwa watalitekeleza wakipata fursa ya kuchaguliwa kuongoza nchi.

Iwapo wapiga kura na hata wananchi kwa ujumla hawatazifahamu na kuelewa ilani hizo watakapochagua mgombea na ikatokea chama chake kikashika madaraka itakuwa vigumu kujua wanachopaswa kumpima kwacho.

Na hata ikitokea akachaguliwa mtu katika ngazi ambayo chama chake hakikuingia madarakani bado ataangaliwa iwapo anasimamia falsafa za ilani ya chama chake katika kuihoji serikali itakayoingia madarakani.

Nimebahatika kuziona ilani za vyama vitatu hadi sasa ambavyo ni ACT-Wazalendo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) na Chama cha Mapinduzi (CCM). Hizi ilani nilizipata baada ya kuzitafuta kwenye tovuti bila mafanikio niliweza kurushiwa kwa njia ya mtandao wa Whatsap na waliokuwa nazo hivyo  natumaini ndizo ilani rasmi.

Ilani hizi kwanza zinatofautiana kwa mwonekano na ukubwa wake. Ilani ya ACT Wazalendo ina kurasa 62 wakati ilani ya Chadema ina kurasa 104 na ile ya CCM ina kurasa 308. Unahitaji uwe na utulivu uweze kuzisoma ilani hizi ili kujua hasa maono yao ni nini na wanatoa mwelekeo gani watakaousimamia wanapoingia madarakani.

Katika uso wa kila Ilani yaani mwanzoni kabisa napo kuna utofauti. Ilani ya  ACT-Wazalendo inaonyesha nembo yao na kisha  maneno ‘ Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2020’ na mwisho wa ukurasa wameweka kauli mbiu yao ‘ Kazi na Bata’ na pembeni yake  sanduku la kupigia kura.

Ilani ya Chadema inaonesha nembo ya chama chao upande wa kushoto mwa karatasi na kulia ndipo walipoandika ‘ILANI YA UCHAGUZI MKUU WA RAISI, WABUNGE NA MADIWANI 2020-2025’. Kwa chini yake zipo picha mbalimbali na mwishoni kauli mbiu ya  ‘Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu,  Chagua Chadema Oktoba 28’.

Ilani ya CCM ukurasa wake wa mbele kuna nembo za chama pande mbili za karatasi  kati ya nembo hizo  maandishi yenye  maneno  ‘ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020’. Kati ya ukurasa  yamerejewa maneno hayohayo  yaliyopo hapo juu na pembeni  yameandikwa maneno ‘TUMETEKELEZA KWA KISHINDO TUNASONGA MBELE PAMOJA’.

Unaweza kujiuliza kwanini ninaanza na mwonekano wa ilani. Nilijifunza wakati fulani kuwa unaweza kutafsirika tofauti kutokana tu na mwonekano. Maneno ya kwanza katika ilani ni muhimu sana kuyaangalia wakati tunafuatilia kujua vyama hivi vinakuja na nini, wakati huohuo tukijiangaliza pia kuwa yote yang’aayo si dhahabu.

Kwenye ilani ya ACT- Wazalendo ukurasa unaofuata una maneno ya ‘TANZANIA  yenye  UCHUMI UNAOPAA na WATU wenye RAHA na FURAHA. Chini ya maneno haya zipo picha mbalimbali. Kwa Chadema ukurasa unaofuata una picha za mgombea urais wa chama hicho na mgombea mwenza wake. Chama Cha Mapinduzi ukurasa uliofuata uko wazi.

Leo nitaziangalia aya chache katika utangulizi na kwa kifupi vipaumbele vinavyooneshwa katika ilani hizo. ACT-Wazalendo imeanza na utangulizi ulioandikwa na  kiongozi wa chama hicho. Maneno ya kwanza kabisa katika utangulizi  yanaonesha maono kuwa   ‘’Tanzania yenye watu wenye hali bora kijamii na furaha ya kweli yenye kujali utu, yenye mfumo mzuri wa utoaji haki, yenye demokrasia ya kweli, yenye uhuru na yenye uchumi jumuishi, imara na unaostawi’’ Hii ndio Tanzania  itakayojengwa na kusimamiwa na Serikali ya ACT-Wazalendo. Uchaguzi huu ni uchaguzi wa kuchagua’’.

Chadema katika utangulizi ilani imeanza na maneno ‘MAENDELEO NA HAKI ZA WATU’ na imeendelea kwa kuelezea kuwa ilani hiyo imetungwa kwa kuzingatia misingi ya falsafa, itikadi pamoja na madhumuni ya kuanzishwa kwa Chadema, falsafa hiyo ikiwa ni ‘ujenzi na udumishaji wa demokrasia na maendeleo nchini vitatokana na nguvu na mamlaka ya umma wa Watanzania, nguvu na mamlaka ya umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa  katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo’. Utangulizi wa ilani ya CCM unaeleza kuwa ‘‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa vyama vya TANU na ASP na baadae CCM, imejengwa katika misingi ya ujamaa na kujitegemea inayozingatia utu, usawa na haki.

“Misingi hii imeimarishwa na siasa safi na uongozi bora wa CCM na imekuwa ndio nguzo ya kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa. CCM itaendelea kuzisimamia Serikali zake kuhakikisha kuwa zinazingatia, kulinda na kudumisha misingi hii adhimu’. Katika utangulizi huu pia ipo kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi tu ! na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.’

ACT-Wazalendo imeainisha vipaumbele 12 ambavyo vimeonyeshwa bayana kuwa ndivyo vipaumbele. Chadema imebainisha mambo ya siku 100 za kwanza. CCM imetiririsha vipaumbele vyake katika sura  nane katika ilani yake.

Kabla ya kuangalia vipaumbele hivyo kuna mambo ambayo ni vyema kuyaangalia katika ujumla wake kama suala la Katiba mpya, Elimu, Afya, Usawa wa Kijinsia n.k.

Kwa leo ninaangalia ilani hizi zinazungumza nini katika suala la Katiba.  Ilani ya ACT-Wazalendo katika sura yake ya pili kifungu 2.4.1, inaeleza kuwa katika kipindi cha miaka miwili katika uongozi wake wa nchi, wakishirikiana na washirika wao watafufua na kukamilisha mchakato wa kuandika Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano.

Chadema katika sehemu ya 2 ya ilani 2. (v) Serikali yao itarejeresha mchakato wa Katiba Mpya kuanzia ilipoishia Rasimu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Warioba.

Katika ilani ya CCM, sikuona kichwa chochote cha habari kinachozungumzia Katiba ila katika aya ya pili kwenye utangulizi wa ilani  ‘CCM  itahakikisha kuwa Tanzania inaendelea kulinda Uhuru wake, kudumisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuimarisha Muungano wetu wenye mfumo wa serikali mbili pamoja na  tunu nyingine za Taifa’.

Kila mtu ana vipaumbele katika kuamua anachagua nani na chama gani ni vyema kuzifuatilia ilani za vyama vyote ili kuweza kuamua. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

0713 337 240

The post Tuzingatie ilani za vyama ili tufanye maamuzi Oktoba 28 appeared first on Gazeti la Rai.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *