img

Sera za fedha, siasa zimefungamana ,on September 17, 2020 at 7:36 am

September 17, 2020

NA ALOYCE NDELEIO  MIJADALA yote inayohusisha fedha ndani ya Bunge huwa ni mizito na hususani inapohusisha pande mbili zinazotofautiana na kila upande kuona kuwa uko sahihi katika hoja zake. Hata hivyo kabla mijadala hiyo haijafikia hatua ya kujadiliwa bungeni majukwaa ya siasa ndiko mijadala hufanyika mara kwa mara na hata kuwa mirefu kuliko inavyokuwa ndani ya
The post Sera za fedha, siasa zimefungamana  appeared first on Gazeti la Rai.,

NA ALOYCE NDELEIO 

MIJADALA yote inayohusisha fedha ndani ya Bunge huwa ni mizito na hususani inapohusisha pande mbili zinazotofautiana na kila upande kuona kuwa uko sahihi katika hoja zake.

Hata hivyo kabla mijadala hiyo haijafikia hatua ya kujadiliwa bungeni majukwaa ya siasa ndiko mijadala hufanyika mara kwa mara na hata kuwa mirefu kuliko inavyokuwa ndani ya Bunge.

Wakati wa kampeni za uchaguzi mbalimbali ndiko mijadala huwa minono kutokana na sababu moja ya msingi kwamba wagombea huwa na ahadi nyingi zinazohusisha matumizi ya fedha.

Mijadala mingi hulenga dhana ya kiuchumi  na mara nyingi ushabiki huwa pembeni kwani kunakuwepo utofauti katika ukokotozi hususani unaohusu taaluma za kifedha na kiuchumi.

Hali hiyo inamaanisha kuwa ni mambo yanayohitaji weledi zaidi kuliko propaganda za hoja nyingine za kisiasa ambazo huegemea zaidi ushabiki wa kiitikadi.

Ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti wa Fedha za Serikali (CAG), zinapotolewa huibua mijadala kuhusu matumizi ya baadhi ya fedha za umma licha ya kwamba linakuwepo deni la taifa.

Kinachogomba katika mijadala ni sera za kifedha, fedha na siasa na inakuwa mirefu, wengine wangetaka ifupishwe. Lakini kiuhalisia ufumbuzi rahisi ni nadra kwani uzito wa mada husababisha ugumu kupata usawa kimizania.

Mageuzi katika fedha za umma kimsingi ni siasa, yana muundo muhimu katika mfumo wa kisiasa, hivyo kuunda mfumo wa siasa za kifedha, kwa lugha ya Kiingereza Fiscal Politics.

Majadiliano ya kisiasa yanasaidia kutatua vikwazo vinavyotokeza na kuwa nguvu ya mabadiliko ya kitaasisi. Hivyo wapanga sera ambao leo wanapuuzia ukweli wa kisiasa huwa si wafanisi.

Mfano ambao ni rejea ya jinsi majadiliano ya kisiasa yalivyoleta mafanikio ni kwa Marekani ambapo miezi 18 kabla ya kufanyika kwa dhifa ya kihistoria wakati George Washington alipoteuliwa kuwa Rais wa Kwanza wa Marekani serikali ya shirikisho ilifilisika.

Hadi Septemba 1789, Idara ya Hazina ilikuwa haijaundwa na mapato ya kwanza ya shirikisho yalikuwa hayajawasilishwa. Hivyo utawala mpya ulitupia jicho ofisi hiyo.

Pamoja na kuyachukua madeni ya majimbo, iliunda upya deni lake la kipindi cha vita kwa kujenga uwezo imara wa kodi katika shirikisho ukiegemea huduma yenye ufanisi ya ushuru wa forodha, kuweka misingi ya deni la umma, kuanzisha benki ya taifa na kukuza maendeleo ya masoko ya kifedha.

Hatua hizo ziliipa serikali ya shirikisho zana za kubeba sera hai za maendeleo ya kiuchumi.

Ni nadra katika historia ya fedha kufanikiwa kwa kipindi kifupi kama hicho. Kujenga na kuunda uwezo wa taifa kusimamia fedha za umma kwa kiwango kikubwa ni mchakato wa kisiasa.

Hilo liliwagawa waasisi wakongwe wa taifa hilo kutoka chama cha Federal, Alexander Hamilton na John Adams waliokuwa wanahamasisha serikali imara ya shirikisho na upande wa pili vyama vya Democratic na Republican vya Jefferson na Madison waliopendelea serikali iliyogwatuliwa na serikali ya shirikisho yenye mipaka yake.

Hamilton alitambua kwamba Katiba yenyewe haingeipa serikali ya shirikisho mamlaka yenye nguvu, hivyo ilikuwa ni muhimu kujenga  miundombinu  ya fedha za umma.

Akiongozwa na dira ya ukweli na imara  kuliko nadharia, Hamilton aliweka programu yake katika ripoti za msingi mitatu: kuhusu deni (Januari 1790), Benki ya Taifa (Desemba 1790) na Viwanda (Desemba 1791).

Ripoti zote ziliangalia maeneo matano ya msingi: kodi, deni la taifa, masoko ya fedha na mashirika, uimara kifedha, kukabili majanga na sera ya biashara.

Kutokana na ripoti ya Hamilton kuwa na ukinzani haikushangaza kwamba hadi Juni 1790, Bunge lilikuwa halijakubali kuridhia madeni ya serikali za  majimbo.

Juni 2 mwaka huo Bunge la Wawakilishi lilipitisha muswada wa fedha bila kugusia deni.

Mgawanyiko ulitokeza; wapi yawe makao makuu ya nchi.  Hamilton alipendelea New York iwe ndicho kituo cha nguvu ya kisiasa na kifedha na ikakubaliwa. Lakini Jefferson na Madison walitaka Potomac.

Hata hivyo makubaliano yalifikiwa Julai 1790, Congress walipopitisha muswada wa Makazi na Mapendekezo kwa mafanikio ya haraka.

Jefferson hata hivyo hakuridhika, zaidi ya miaka miwili baadaye Septemba 1792, Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Nje alirejea suala hilo katika barua aliyomwandikia Rais Washington kuhusu mkanganyiko anaokutana nao kuhusu sera zilizowekwa hazina.

Migongano ya mwanzo ya kisera kati ya kambi mbili yalikuwa ni alama ya tofauti za kimsingi.

Mwaka 1792 Madison na Jefferson walianzisha kambi yao ya kushindana na kambi ya chama cha Federal.

Uamuzi huo uliwezesha kuanza kwa uanataaluma, siasa za ushindani kivyama kama jiwe la msingi la uwakilishi kidemokrasia Marekani.

Mkakati huo wa awali ulikuwa ni mfano dhahiri ulioonesha  siasa za kifedha zinaweza kuandika historia.

Sera za kifedha, fedha na siasa ni mambo mawili  yasiyoachanika, na ndio ukweli uliopo kwa deni, kodi na uwezo wa nchi.

Jambo linalobakia kuwa wazi ni kwamba siasa zina mchango muhimu katika kuyafikia mageuzi ya muda mrefu ya fedha za umma.

Mageuzi katika fedha hizo yamo katika misingi ya kisiasa na yamekuwa yanaunda taswira muhimu pia katika mfumo wenyewe wa kisiasa.

Majadiliano au mijadala ya kisiasa yanaweza kusaidia kukabiliana na vikwazo vinavyoonekana kuwa ni vigumu kupata ufumbuzi na kuwa ni msukumo wa mabadiliko kitaasisi.

Wapanga sera ambao hupuuzia uhalisia huo wa kisiasa hujikuta wakiwa ni watu wasioaminika.

Aidha ni katika mazingira hayo ya majadiliano ya kisiasa masuluhisho kuhusu madeni yanayoikabili nchi yanaweza kuwekewa mikakati ya kuyalipa.

Aidha pale inapoonekana kuwa mzigo wa madeni ni mkubwa inaweza kuwepo mikakati ya kuomba msamaha au kupunguziwa mzigo wenyewe.

Hilo linaenda bega kwa bega na kuimarisha ukusanyaji wa kodi na kuangalia  vikwazo vinavyokwamisha upatikanaji wa mapato ya serikali.

Katika mazingira hayo ndipo linaweza kuwepo hitimisho kuwa uwezo wa nchi kiuchumi upo katika hali ipi na mkazo wa kuufanya uwe endelevu uwekwe katika maeneo gani.

The post Sera za fedha, siasa zimefungamana  appeared first on Gazeti la Rai.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *