img

Yanga yamaliza utata jezi za msimu mpya, on September 12, 2020 at 9:08 am

September 12, 2020

 ZAINAB IDDY – DAR ES SALAAM  HATIMAYE kiu ya muda mrefu ya mashabiki wa Yanga kuiona jezi itakayotumiwa na timu hiyo katika msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, imemalizika baada ya kuanikwa hadharani jana.  Jezi hizo zilizinduliwa jana Makao Makuu ya klabu hiyo,yaliyoko mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.  Jezi zilizozinduliwa,

 ZAINAB IDDY – DAR ES SALAAM 

HATIMAYE kiu ya muda mrefu ya mashabiki wa Yanga kuiona jezi itakayotumiwa na timu hiyo katika msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, imemalizika baada ya kuanikwa hadharani jana. 

Jezi hizo zilizinduliwa jana Makao Makuu ya klabu hiyo,yaliyoko mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam. 

Jezi zilizozinduliwa ni kwa ajili ya michezo ya nyumbani ambayo itatumia rangi ya kijani, ugenini(njano) na bluu ambayo itatumika pale itatokea kushabihiana na za wapinzani wao. 

Ikumbukwe kwamba, awali klabu hiyo ilikuwa izindue jezi za msimu mpya wakati wa kilele cha tamasha lake la Wiki ya Mwananchi, kilichofanyika Agosti 30, mwaka huu. 

Lakini kutokana na kile kilichoelezwa na uongozi wa Yanga,vikwazo vya kusafirisha mizigo vinavyotokana na janga la corona, mpango wa kuzindua jezi hizo tarehe hiyo ulishindikana. 

Hata hivyo, mashabiki wengi wa klabu hiyo hawakuridhishwa na sababu zilizotolewa kukwamisha uzinduzi wa jezi hizo na kuhisi huenda walihadaiwa na uongozi wao. 

Kilichokuwa kinawakera zaidi mashabiki wa klabu hiyo, wapinzani wao wakubwa, timu ya Simba ilifanikiwa kuzindua jezi zake kabla ya msimu mpya kuanza. 

Akizungumza wakati wa tukio hilo lililoenda sambamba na uzinduzi wa duka la vifaa vya michezo la klabu hiyo, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM,inayoidhamini Yanga, Mhandisi, Hersi Said,alisema wamezingatia ubora katika utengenezaji wa jezi hizo. 

“Jezi hizi zimetengenezwa kwa kuzingatia viwango vya ubora ili Wanayanga watakaponunua iendane na thamani ya fedha walizotoa. 

 “Leo tumezindua jezi za nyumbani ambayo ni tisheti ya kijani na bukta nyeusi, wakati za ugenini ni tisheti ya njano na bukta nyeusi lakini pia zipo nyingine za dharura zitakuja kuzindulia siku chache zijazo,”alisema Said. 

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Yanga,wakiwongozwa na Makamu Mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utendaji. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *