img

Watia nia jimbo la Hai wamuunga mkono Saashisha Mafuwe, on September 12, 2020 at 12:47 pm

September 12, 2020

Mwandishi wetu Aliyekuwa mtia nia wa kugombea Ubunge Jimbo la Hai kupitia Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Shabani Mwanga, ametangaza rasmi kuungana na mgombea aliyepitishwa na chama hicho katika jimbo hilo, Saashisha Mafuwe. Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mwanga amesema hilo ndilo jambo lao walilo kubaliana na wenzake 41, waliokuwa katika kinyang’anyiro,

Mwandishi wetu

Aliyekuwa mtia nia wa kugombea Ubunge Jimbo la Hai kupitia Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Shabani Mwanga, ametangaza rasmi kuungana na mgombea aliyepitishwa na chama hicho katika jimbo hilo, Saashisha Mafuwe.

Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mwanga amesema hilo ndilo jambo lao walilo kubaliana na wenzake 41, waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho na kuamua kumuunga mkono Mafuwe.

“Wote tuliokuwa katika kinyang’anyiro cha Ugombea Ubunge tumekubaliana kuungana na Mafuwe ili kumuondoa maradakani Mbunge wa Chadema, Freeman Mbowe aliyekaa kwenye jimbo hilo miaka 15 sasa.

“Wananachi wa Jimbo la Hai wanstakiwa kumchagua Saashisha kwa ajili ya maendeleo ya haraka katika jimbo hilo na kuwataka  kumchagua Dkt. John Magufuli katika nafasi ya Uraisi ili aendeleze mazuri yasiyo na mfano aliyofanya ndani ya kipindi kifupi aliyokaa madarakani.”anasema Mwanga

Pia anasema “Jimbo hilo limekuwa nyuma kwa muda mrefu kutokana na kuongozwa na Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema na amekuwa akitumia muda mwingi kukipigania chama chake na kulisahau jimbo.” 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *