img

Kanye West atajwa ‘Keeping Up With Kardashians’ kusimama, on September 12, 2020 at 9:18 am

September 12, 2020

 LOS ANGELES, MAREKANI  MAPEMA wiki hii mwanamitindo nyota duniani, Kim Kardashian, aliweka wazi kuwa kipindi cha Keeping Up With The Kardashians (KUWTK), kitafikia mwisho mwaka ujao baada kuonekana kwenye televisheni E! kwa miaka 14 mfululizo.  Mrembo huyo mwenye miaka 39, hakuweka wazi sababu kubwa ya kufikia maamuzi hayo huku mtandao wa TMZ ukidai chanzo ni,

 LOS ANGELES, MAREKANI 

MAPEMA wiki hii mwanamitindo nyota duniani, Kim Kardashian, aliweka wazi kuwa kipindi cha Keeping Up With The Kardashians (KUWTK), kitafikia mwisho mwaka ujao baada kuonekana kwenye televisheni E! kwa miaka 14 mfululizo. 

Mrembo huyo mwenye miaka 39, hakuweka wazi sababu kubwa ya kufikia maamuzi hayo huku mtandao wa TMZ ukidai chanzo ni Kourtney Kardashian, Kylie Jenner na Kim mwenyewe. 

Kipindi hicho kilikuwa kinaangazia maisha halisi ya familia ya Kardashian ambapo wahusika waliojizolea umaarufu ni mama yao Kris Jenner, Khloe Kardashian, Rob Kardashian na Kendall Jenner. 

TMZ wamesema Kim amekuwa chanzo kwa sababu mume wake, Kanye West kuingia kwenye siasa ambapo anawania urais baadaye mwaka huu hivyo mrembo huyo hatakiwi kuyaanika maisha yake kwa kuwa kitendo hicho kinaweza kuwa na madhara hapo baadae endapo mumewe atafanikiwa kuwa rais wa Marekani. 

 Kwa upande mwingine Kylie anataka kupindi hicho kifikie tamati kwa kuwa anaingiza fedha nyingi kupitia biashara ya bidhaa za urembo, hivyo anataka muda mwingi kuutumia kwenye mambo yake yanayomwingizia fedha. 

Kourtney yeye anatajwa kama chanzo kwa kuwa anataka kutumia muda mwingi kukaa na familia yake yenye watoto watatu Mason, Reign na Penelope. 

KUWTK ni miongoni mwa vipindi vichache ya runinga vyenye mamilioni ya mashabiki kote ulimwenguni huku kikijizolea tuzo kibao kama Teen Choice Awards, People’s Choice AwardsE! , People’s Choice Awards na nyingine nyingi. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *