img

Ruto ‘aongezewa nguvu’ mbio za urais Kenya,on September 3, 2020 at 6:41 am

September 3, 2020

NA ISIJI DOMINIC NI kitendawili ambacho ni kigumu kutengua hususan Wakenya wanapojiuliza nani atakayemrithi Rais Uhuru Kenyatta pindi atakapomaliza muda wake madarakani. Ilikuwa rahisi kubaini nani atakayevaa viatu vyake wakati wa uchaguzi wa mwaka 2013 pale Rais Uhuru na Naibu Rais William Ruto walipounganisha vyama vyao na kuunda muungano wa Jubilee uliopambana dhidi ya muungano
The post Ruto ‘aongezewa nguvu’ mbio za urais Kenya appeared first on Gazeti la Rai.,

NA ISIJI DOMINIC

NI kitendawili ambacho ni kigumu kutengua hususan Wakenya wanapojiuliza nani atakayemrithi Rais Uhuru Kenyatta pindi atakapomaliza muda wake madarakani.

Ilikuwa rahisi kubaini nani atakayevaa viatu vyake wakati wa uchaguzi wa mwaka 2013 pale Rais Uhuru na Naibu Rais William Ruto walipounganisha vyama vyao na kuunda muungano wa Jubilee uliopambana dhidi ya muungano wa Cord wakati huo chini ya kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka (Wiper-Kenya) na Moses Wetangula (Ford-Kenya).

Ni uchaguzi ambao matokeo yake yalipingwa mahakamani lakini aliyekuwa Jaji Mkuu, Dk. Willy Mutungi, baada ya kusikiliza kesi hiyo, yeye na jopo lake la majaji wa upeo wa juu walijidhihirisha Uhuru na Ruto walishinda kihalali hivyo kuruhusu wawili hao kuapishwa.

Viongozi hawa wawili walikuwa na ukaribu na mara kadhaa katika majukwaa ya siasa walinukuliwa wakijinasibu baada ya miaka 10 ya Uhuru uongozini, miaka mengine 10 itakuwa zamu ya Ruto. Uhuru alifanikiwa kutetea tena nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu 2017.

Huku akiwa amebakisha takribani miaka miwili kabla ya kuondoka madarakani, Rais Uhuru amenukuliwa akisema chaguo la mrithi wake litawashangaza wengi hivyo kumweka njia panda Ruto hususan na kile kinachodaiwa mpango wa kukiuka makubaliano ya mwaka 2013.

Aidha muafaka kati ya Rais Uhuru na Raila Machi 8 mwaka 2018 yanazidi kumweka ‘gizani’ Naibu Rais Ruto kutokana na kutohusishwa katika majadiliano yanayadaiwa kulenga kuwaunganisha Wakenya.

Tofauti ambazo sasa zinaonekana wazi kati ya viongozi hao wawili wa juu imewaibua wachambuzi wa masuala ya siasa wakidai ndiyo inayochochea Naibu Rais kuanza kutafuta njia mbadala kutimiza azma yake ya kuwa Rais wa Awamu ya Tano Kenya.

Mara kadhaa Ruto na washirika wake wamekuwa wakitoa kauli ambazo zinakinzana na Serikali na hii imepelekea Rais Uhuru kufanya mabadiliko ya viongozi na wajumbe wa kamati mbalimbali ndani ya Bunge la Taifa na Bunge la Seneti.

Aidha baadhi ya majukumu yaliyokuwa yakifanywa na Naibu Rais mengi yapo chini ya Waziri wa Usalama Dk. Fred Matiang’I, jambo ambalo linapelekea baadhi ya wanasiasa kumshinikiza Ruto kujiuzulu ili ajipange kuelekea uchaguzi mkuu 2022, lakini Naibu Rais ameamua kuzipuuza kwasasa.

Kuna wanasiasa tena kutoka kambi ya upinzani ambao wamekuwa wakimpigia debe Ruto kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika miaka miwili baadaye. Kwa hali ilivyo kwasasa katika siasa za Kenya, ni ngumu kujua nani yupo Serikalini na nani upinzani.

Ndani ya Serikali kuna wanaopinga hoja za Serikali wakati ndani ya upinzani kuna wanaounga mkono hoja za Serikali. Imani ya Wakenya kwa upinzani kufuatilia na kuhoji mambo yanayofanywa na Serikali imeanza kufifia.

Chama tawala na muungano wa upinzani, NASA, zote zipo kwenye mvutano wa ndani kwa ndani na hii ni ishara huenda Wakenya wakashuhudia miungano mipya ya siasa kuelekea uchaguzi mkuu 2022.

Kuna baadhi ya wanasiasa waandamizi kutoka chama cha Jubilee, mmoja wao akiwa Makamu Mwenyekiti, David Murathe, wameweka wazi azma yao ya kumuunga mkono Raila kuwania urais uchaguzi mkuu wa 2022.

Katika kile kinachoonekana kujibu mapigo, waliyokuwa katika mstari wa mbele kumfanyia kampeni Rais Uhuru na kiongozi wa ODM, Raila, wakati wa uchaguzi mkuu 2017, sasa wamehamisha nguvu zao kwa Naibu Rais Ruto kuelekea 2022.

Hao ni maseneta wa zamani Johnson Muthama, Dk. Boni Khalwale na waziri wa zamani wa nishati, Davis Chirchir. Muthama na Khalwale walikuwa watu muhimu sana kwa wagombea urais kupitia muungano wa NASA ambao ni Raila na Kalonzo.

Muthama na Dk. Khalwale walikwepo kwenye kamati ya uratibu wa taifa ikiwa ni chombo cha pili cha juu cha maamuzi kwenye muungano wa NASA ambaye pia mwenyekiti mwenza alikuwa Seneta wa Siaya, James Orengo. Majukumu yao yalikuwa ni kushughulikia kampeni ya kila siku ya Raila.

Chirchir naye anadaiwa kuhamia kambi ya Naibu Rais Ruto ukizingatia waziri huyu wa zamani alikuwa wakala mkuu wa Rais Uhuru wakati wa uchaguzi mkuu 2017.

Mbali ya kuwa wakala mkuu, Chirchir alishawahi pia kuwa mjumbe tume ya uchaguzi Kenya na inadaiwa uwepo wake katika kambi ya Naibu Rais inahusishwa na kutengeneza manifesto na mbinu zingine za kampeni ikiwemo miundombinu ya teknolojia.

Uwepo wa Muthama kwenye kambi ya Ruto ni nguzo muhimu ukizingatia ushawishi aliyonayo kwa jamii ya Wakamba. Hii ni eneo ambayo Ruto atahitaji kupata kura endapo atajitosa kuwania urais 2022.

Muthama ambaye ni seneta wa zamani wa Machakos ametofautiana na aliyekuwa Makamu wa Rais Kalonzo na yeye (Muthama) pamoja na Dk. Khalwale na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wiper, Hassan Omar, wameamua kumtetea Ruto wakitoa matamko ambayo hata viongozi waliochagulia na wanaomuunga mkono Naibu Rais wanahofia kuzungumza.

“Kwa kuwa sisi sio viongozi tuliochaguliwa na hatujateuliwa katika ofisi yoyote, hatuna mzigo wa ziada kama wale ambao wanashikilia ofisi hizo katika uongozi na kutumia mamlaka yao kumuadhibu yeyote anayemuunga mkono Naibu Rais. Hivyo basi tunakuwa na uhuru wa kuongea masuala nyeti yanayohusu serikali paispo kuwa na uoga,” alisema Dk. Khalwale.

Muthama alijiondoa katika uchaguzi mkuu 2017 kutokana na tofauti zake na Kalonzo huku Dk. Khalwale akishindwa na Wycliffe Oparanya katika nafasi ya ugavana wa Kakamega naye Omar akibwagwa na Hassan Joho nafasi ya ugavana wa Mombasa.

Mpasuko ndani ya chama tawala impelekea kambi ya Naibu Rais kufungua ofisi sambamba na ile ya makao makuu ya Chama cha Jubilee huku Naibu Katibu Mkuu wa Jubilee, Caleb Kositany ambaye pia ni Mbunge wa Soy katika Bunge la Taifa, na aliyekua Kiongozi wa Wengi Bunge la Seneti, Kipchumba Murkomen, wakitwishwa majukumu ya kushawishi uungwaji mkono bungeni.

“Wale ambao wanadhani kwamba Ruto yupo pekee yake wamekosea sana. Hayuko pekee yake. Nataka niwaambie Wakenya kwamba Ruto hayuko pekee yake. Hajatengwa,” Muthama aliliambia moja ya chombo cha habari nchini Kenya.

“Tutakuwa kwa ubora wetu baada ya janga la corona kupita kwa lengo la kumtangaza kwa Wakenya.”

Katika kile ambacho kinaonekana tayari kupambana na vizingiti vyovyote vilivyo mbele yake, Naibu Rais Ruto alisema hatishiwi na kile kinachoitwa ‘Deep State’ au ‘mfumo’ katika azma yake ya kumrithi Rais Uhuru 2022.

‘Deep State’ haina tofauti na serikali ndani ya serikali, na hii ni aina ya utawala unaoundwa na mitandao ya nguvu inayofanya shughuli zake za kisiasa kwa uhuru ndani ya serikali katika kutekeleza ajenda na malengo yao wenyewe.

Ruto aliithubutu ‘deep state’ ambayo inajumuisha watu wenye ushawishi mkubwa serikalini akiishutumu kupanga njama kuhakikisha anashindwa kufaulu katika mipango yake ya kumrithi Rais Uhuru.

Naibu Rais aliifananisha njama hizo na vitisho walivyopokea yeye na Rais Uhuru kuelekea uchaguzi mkuu 2013. Aliwakumbusha Wakenya namna walivyokuwa wanaambiwa ‘kila chaguo lina matokeo’.

Ilikuwa wakati wawili hao, Uhuru na Ruto, walipokuwa wanakumbwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) iliyopo The Hague nchini Uholanzi.

The post Ruto ‘aongezewa nguvu’ mbio za urais Kenya appeared first on Gazeti la Rai.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *