img

KANYE WEST ADAI NI TAJIRI KULIKO TRUMP, on September 2, 2020 at 9:44 am

September 2, 2020

 NEW YORK, MAREKANI  NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, amedai hakuna mtu ambaye anaweza kumlipa kwa kuwa ana fedha za kumzidi rais wa nchi hiyo Donald Trump.  Mapema wiki hii msanii huyo alifanya mazungumzo na nyota wa muziki huo Nick Cannon katika kipindi chake cha ‘Cannon’s Class’ na kisha akaanza kutamba,

 NEW YORK, MAREKANI 

NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, amedai hakuna mtu ambaye anaweza kumlipa kwa kuwa ana fedha za kumzidi rais wa nchi hiyo Donald Trump. 

Mapema wiki hii msanii huyo alifanya mazungumzo na nyota wa muziki huo Nick Cannon katika kipindi chake cha ‘Cannon’s Class’ na kisha akaanza kutamba kuwa ana fedha nyingi. 

“Kaka, hakuna mtu ambaye anaweza kunilipa, niweke wazi kuwa nina fedha nyingi zaidi ya rais Trump,” alisema rapa huyo. 

Kanye West ni msanii ambaye amejitokeza kwenye mbio za kuwania urais nchini Marekani mwaka huu na anatajwa kuwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 5.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *